Wednesday, December 29, 2010

NA HILO NALO JAMANI DU! HII KWELI TANZANIA.

Waswahili husema ukiona za helea hujue zimeundwa  napata hushangao kuwa  kwanini suala la KATIBA linapigwa danadana? na kulipuuzia kanakwamba si msingi imara wa uongozi?.Bila ya unafiki viongozi waliopewa dhamana  ya kuliongoza  tai?fa hili na wananchi wenyewe wanataka katiba mpya  .Wao wanasema haiwezekani kwani kipi kinawezekakana kwa TZ ? IKIWA KILA KITU HAIWEZEKANI JAMANI? hatakubadilisha katiba?! acheni unafiki  ni wakati wa mabadiliko viongozi wetu lazima mtamue hilo.Mbona mnangangania mfumo uleule wa tangu mwanzo na sasa na siku zote na milele amina? je katiba ya mwaka 1977 haijapita na wakati?.Tuishi kulingana na wakati na sio kulingana na matakwa ya wachache.Uma unataka katiba basi tupeni katiba mpya.NA wala msije kutumia nguvu ya dola kulizima suala la katiba.Jiulizeni jamani wafuasi wa CUF tu wamejaribu kuandamana kushinikiza kuandikwa kwa katiba mpya lakini polisi ambao jukumu lao kubwa ni kulinda amani lakin wao wamekuwa kipawa mbele ktk kuzuia sauti ya watanzania kuhusu katiba.Tumeshudia mbunge Ubungo ,bwana Mnyika akipeleka hoja binafsi ofisi ndogo ya mbunge Dar-es salaam.Naamini yeye ni mwakilishi wa mawazo ya wananchi wake  waliomchagua.TUNAOMBA VIONGOZI MSIWE WABABAISHAJI  maana wananchi ndio tunao umia.WAtanzania  tujiulize je tunayo DEMOKRASIA AU KIVULI CHA DEMOKRASIA?  

No comments:

Post a Comment